Kocha wa zamani wa Mamelod Sundowns na Al Ahly Pitso Mosimane bado hajasahau shamrashamra za wiki ya Mwananchi ambayo aliishuhudia akiwa mgeni mwalikwa
Jambo analolikumbuka zaidi ya 'tetema' ya mshambuliaji Fiston Mayele aliyoishuhudia ikirindima uwanja mzima wakati wa utambulisho wa Mayele
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Mosimane amebainisha bado anakumbuka tukio hilo

"Nilipoalikwa kwenye siku ya Wananchi nilifanikiwa kushuhudia mtindo maarufu wa kushangilia. Niamini mimi, Uwanja mzima ulisimama na kuiga, hali hiyo imeendelea kusalia kwenye mfumo wangu hadi leo. Pongezi kwa soka la Tanzania," aliandika Mosimane
Huo ulikuwa mwanzo wa msimu mzuri kwa Mayele ambaye katika mechi saba zilizofuata baada ya wiki ya Mwananchi, ametetema mara 12
Huu ni msimu ambao Afrika nzima itatambua staili hiyo ya kutetema kwani Wananchi wamepania kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa