Hii Yanga sio ya kutishiwa 'nyau'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2022
Hii Yanga sio ya kutishiwa 'nyau'

Huko mitandaoni maandiko ya kuipamba Al Hilal yanaendelea kushika kasi baada ya kupangwa kucheza na Yanga katika raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa

Jana Al Hilal walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya St George na hivyo kutinga raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya St George

Maandiko hayo yana lengo ya kuitisha/kuikatisha tamaa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya timu hiyo

Mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa Oktoba 08 na mchezo wa marudiano ni Oktoba 14

Jambo moja la uhakika ni kuwa Yanga imejipanga sawasawa kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu

Ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Zalan Fc ni ishara ya dhamira ya Wananchi kuelekea michuano hiyo

Najua watasema Zalan Fc ni dhaifu lakini hata hao wanaowapamba kila siku wameshaonja kipigo cha Yanga msimu huu

Wananchi msitishwe na hizo makala kwani Yanga hii ya Profesa Nabi inaweza kumfunga yeyote hapa Afrika

Historia haichezai mpira, hayo mambo yaliyopita hayana nafasi kwa sasa, muhimu ni maandalizi tu

Tuliwaona St George walipokuja kucheza na Simba hapa Tanzania, wakafungwa mabao 2-0 na pia tuliwaona Al Hilal walipocheza na Simba kule Sudan wakashinda 1-0

Al Hilal wamelazimika kufuzu kupitia bao la ugenini dhidi ya St George, halafu hawa ndio muwatishie Yanga kweli?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’