Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza maamuzi ya kamati hiyo kuhusiana na hukumu ya Haji Manara ya kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na kutakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 20.
Mwenyekiti wa kamati hiyoΒ Richard Mbaruku amesema wamepitia rufaa ya Manara na kuona kuwa inakosa mashiko ila wametumia busara ya kumpunguzia adhabu na sasa atatumikia adhabu yake ya miaka miwili na faini ya Tsh milioni 10 kutoka Tsh milioni 20 iliyokuwa awali
ADVERTISE HERE