Yanga imepanda kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Vijana wa kocha Nasreddine Nabi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 yakiwekwa kambani na Djuma Shabani kupitia mpira wa adhabu na Fiston Mayele alioyefunga moja ya mabao bora msimu huu mpaka sasa
Kipindi cha pili vijana wa Nabi walipunguza kasi kidogo lakini wakamaliza mchezo kibabe kwa Stephane Aziz Ki kufunga bao la tatu kwenye dakika za majeruhi
Shuti lake la mguu wa kushoto kutoka nje kidogo ya 18 lilimchanganya Faroukh Shikhalo na kujaa kimiani
Ni ushindi wa tatu katika michezo minne ya ligi msimu huu, ukiwa ni mchezo wa 41 Yanga inacheza pasipo kupoteza



ADVERTISE HERE