Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa raundi ya nne
Ni mchezo muhimu kwa Wananchi kupata ushindi baada ya kupata sare kwenye mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc
Habari njema kwa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ni kuwa leo atakuwa na kikosi chake kamili, mchezaji mmoja tu mlinda lango Djigui Diarra ambaye atakosekana akiwa majeruhi
Mtibwa Sugar wamekuwa na msimu mzuri mpaka sasa wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama saba kama ilivyo kwa Yanga lakini wao wakiwa wamefunga mabao mengi zaidi
Ni wazi utakuwa mchezo mkali lakini kwa Yanga wanahitaji kushinda ili kusogea kileleni mwa msimamo wa ligi
Mchezo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku