Mshambuliaji Crispin Ngushi hatoichezea Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya jina lake kutosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema Ngushi amekuwa akisumbuliwa na majeraha hivyo waliona ni vyema nafasi yake kuiweka kwa ajili ya dharura, anaweza kusajiliwa kushiriki hatua itakayofuata kama Yanga itatinga makundi
Juzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliweka hadharani kikosi cha Yanga kilichosajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF
Kikosi hicho cha wachezaji 27 waliosajiliwa kinaundwa na makipa Abutwalib Mshery, Johora Erick na Djigui Diarra wakati mabeki ni Hamad Ibrahim,David Brayson, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Lomalisa Mutambara, Kibwana Shomari, Djuma Shaban na Abdallah Shaibu.
Viungo ni Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Salum Abubakar, Faridi Musa, Feisal Salum, Yannick Bangala, Aziz Ki na Ducapel Moloko wakati washambuliaji ni Yusuph Athuman, Fiston Mayele, Bernard Morrison, Lazarous Kambole, Denis Nkane, Heritier Makambo na Dickson Ambundo