MatchDay : Yanga vs Azam Fc, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2022
MatchDay : Yanga vs Azam Fc, NBC PL

Baada ya mapumziko ya kalenda ya CHAN, ligi kuu ya NBC inarejea leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga wataumana na Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku

Ni dabi ya jijini Dar es salaam, ukitoa mchezo wa watani wa jadi, mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc unashika nafasi ya pili kwa ukubwa

Nje ya uwanja, mashabiki wa Yanga wanaamini Azam Fc na Simba ni kama kaka na dada hivyo ushindi dhidi ya Azam Fc utapeleka maumivu Msimbazi na ni hivyo hivyo kinyume chake, ushindi kwa Azam utapeleka furaha Msimbazi

Mara nyingi timu hizi zinapokutana mchezo huwa sio mwepesi, dakika 90 ndizo zinazoamua matokeo

Yanga imeweka rekodi ya kucheza mechi 39 pasipo kupoteza, lakini timu ya mwisho kuifunga Yanga ni Azam Fc, April 25 2021 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ulikuwa mchezo wa kwanza na pekee kwa Kocha Nasreddine Nabi kupoteza tangu alipojiunga na Yanga mwanzoni mwa April 2021

Nabi amesema licha ya kikosi chake kushinda mechi zote mbili msimu uliopita, hawapaswi kubweteka kwani watahitaji kupambana ili kuweza kushinda siku ya leo

Wakati Yanga kikosi chao kina mabadiliko madogo, Azam Fc wamefanya usajili mkubwa wakisajili nyota wengi mahiri

Hata hivyo Azam Fc walianza msimu kwa kusuasua wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja katika dimba lao la Azam Complex matokeo yaliyopelekea kufanya mabadiliko ya benchi lao la ufundi

Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza katika uwanja wake wa nyumbani kwenye ligi msimu huu, michezo miwili ya kwanza walicheza mkoani Arusha dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union na kufanikiwa kushinda yote

Mtanange utapigwa kuanzia saa moja usiku

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’