Winga wa Yanga Tuisila Kisinda ametua nchini kuanza majukumu yake katika kikosi cha Yanga
Yanga imemrejesha Kisinda akitokea klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco

Mkurugenzi wa Mashindano klabu ya Yanga Saad Kawemba amesema wamemsajili Kisinda kwa ajili ya kumtumia kwenye mashindano ya ndani na michuano ya Kimataifa
Taratibu za usajili wake zilikamilika ndani ya dirisha la usajili ikiwa ni pamoja na kupata ITC yake, Yanga ikimbadilisha na Lazarus Kambole kwa ajili ya ligi ya ndani
Kisinda pia amesajiliwa kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa ambayo awamu ya pili ya dirisha la usajili litafungwa Septemba 15
Yanga imelazimika kulipa faini ili kumsajili kwenye mfumo wa CAF lakini ataruhusiwa kutumika kuanzia hatua ya makundi
ADVERTISE HERE