Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limebainisha kuwa usajili wa wachezaji wa kigeni hasa kwa timu ambazo zinashiriki mashindano ya Kimataifa ulishapitishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho hili
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji katika mazingira maalum ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji hao wa kigeni ili wawahi dirisha la usajili wa CAF
Wachezaji wa timu zinazoshiriki Kimataifa, Yanga, Simba, Azam Fc na Geita Gold walipewa leseni kwa ajili ya msimu wa 2022/23 ambazo zilitumika kuwaombea usajili kwa ajili ya mashindano ya CAF
Kwa mujibu wa kanuni ya 62(1) ya ligi toleo la 2022 klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12
ADVERTISE HERE