Kuna uwezekano mkubwa kama Yanga itavuka hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, itakutana na Al Hilal ya Sudan katika raundi ya kwanza
Septemba 9 Yanga itacheza na Zalan Fc katika mchezo wa kwanza hatua ya awali, mechi ikitarajiwa kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Zalan Fc wakiwa wenyeji
Mchezo wa pili utapigwa wiki moja baadae hapo hapo katika dimba la Mkapa Yanga wakiwa wenyeji
Al Hilal watacheza na St George ya Ethiopia katika mchezo wa awali wakianzia ugenini kule Ethiopia na mchezo wa marudiano kupigwa Sudan
Al Hilal wananolewa na kocha wa zamani wa AS Vita Florente Ibenge ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea klabu ys RS Berkane
Ibenge atakumbana uso kwa uso na wachezaji watano aliowahi kuwafundisha katika klabu ya AS Vita
Joyce Lomalisa, Djuma Shaban, Yannick Bangala, Jesus Moloko na Fiston Mayele wote wamewahi kufundishwa na Ibenge
Hautakuwa mchezo mwepesi lakini kwa hakika Wananchi watahitaji kushinda ili kutinga hatua ya makundi
Yanga inaendelea na maandalizi mkakati ukiwa kuvuka hatua ya awali kwanza kabla ya kufikiria mpinzani watakayekutana nae katika raundi ya kwanza