Niyonzima aitabiria Yanga makubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2022
Niyonzima aitabiria Yanga makubwa

Kiungo na nahodha wa zamani wa Yanga Haruna Niyonzima amesema anaipa nafasi timu yake hiyo ya zamani kutetea ubingwa wa ligi kuu waliotwaa msimu uliopita

Niyonzima ambaye hivi karibuni alikuwa nchini na timu ya Taifa ya Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya CHAN dhidi ya Ethiopia, amesema anaiona Yanga ikiwa bora zaidi kuliko wapinzani wake katika mbio za ubingwa baada ya usajili makini uliofanyika huku pia wakiwa na wachezaji wote waliokuwa nao msimu uliopita

"Nafikiri Yanga bado wako vizuri sana. Msimu uliopita walifanya mapinduzi kwa kuweka pesa na kusajili wachezaji bora ambao waliungana na kuwa kitu imara kisha kuipiku Simba" 

"Msimu huu pia wamejipanga sana, wameweza kubakisha mastaa wao wote wa msimu uliopita na kuongeza wengine bora hivyo watasumbua sana na kwa nilivyoiona ligi hadi sasa ni ngumu kuizuia Yanga kuwa bingwa," alisema Niyonzima

Niyonzima aliitumikia Yanga kwa takribani misimu sita kabla ya kusajiliwa na Simba aliyoitumikia kwa misimu miwili na baadae kurejea tena Yanga ambako alicheza kwa msimu mmoja

Kwa sasa Niyonzima anaichezea AS Kigali ya kwao Rwanda, amehusishwa kuhitajika na matajiri wa Singida Big Stars ambao hata hivyo inaonekana mpango wa kumsajili haukufanikiwa

Dirisha la usajili litafungwa Jumatano, August 31 2022

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’