Klabu ya Zalan Fc, mabingwa wa ligi kuu ya Sudan Kusini huenda wakatumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wao dhidi ya Yanga hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) halijaidhinisha uwanja wowote kutoka Sudan Kusini kutumika kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kwa kuwa havikidhi vigezo
Hii itakuwa habari njema kwa Yanga, kwani kama wataidhinishwa kutumia dimba la Mkapa, mechi zote mbili zitapigwa katika uwanja huo
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Septemba 09-11 wakati mchezo wa mkondo wa pili utapigwa wiki moja baadae
Timu itayoshinda kwenye raundi ya kwanza itakumbana na mshindi kati ya St George dhidi ya Al Hilal ya Sudan
ADVERTISE HERE