Baada ya ujio wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye ameonekana kuyamudumu vyema majukumu ya namba 10, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amelazimika kufanya mabadiliko katika kikosi chake cha kwanza kwa kumrudisha Feisal Salum 'Fei Toto' chini kabisa katika eneo la kiungo
Feisal amerejea katika majukumu ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya ujio wa Nabi, ameendeleza ubora wake katika eneo hilo
Jana katika mchezo dhidi ya Coastal Union, Feisal alianza kwenye eneo la kiungo na Khalid Aucho yeye akiachiwa majukumu ya kuchezesha timu kutokea chini
Kwa ubora anaonyesha Feisal katika nafasi hiyo ni wazi anampa mtihani mwingine Nabi
Yannick Bangala, Aucho, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Sure Boy na Feisal wote wanamudu kucheza katika nafasi hiyo
Kwa hakika msimu huu Nabi anafurahia ubora wa kikosi chake, ana kikosi chenye watu kwelikweli katika kila nafasi