Wananchi wako tayari kuikabili Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2022
Wananchi wako tayari kuikabili Coastal Union

Kikosi cha Yanga jioni ya leo kimekamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali, utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha

Baada ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, Yanga iliendelea kubaki mkoani Arusha kusubiri mchezo huo ambao Coastal Union ni wenyeji

Coastal wamechagua kutumia dimba la Sheikh Amri Abeid baada ya uwanja wao wa Mkwakwani kufungiwa

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kitawakosa wachezaji watatu Lazarus Kambole, Djigui Diarra na Salum Abubakar ambaye aliumia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba

Nae Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amewashukuru mashabiki wa mkoani Arusha kwa kuwapa mapokezi mazuri na kuendelea kuwaunga mkono

Kaze amesema mashabiki watarajie mambo mazuri kutoka kwa timu yao kwani msimu huu watakuwa na kikosi bora pengine kuliko msimu uliopita

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’