Lomalisa, Gael kuanza leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Aug 2022
Lomalisa, Gael kuanza leo?

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi huenda leo akafanya mabadiliko ya kikosi chake kitakachoikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa siku ya Jumamosi ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, Nabi hakuwatumia baadhi ya nyota wake wapya

Mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa, kiungo Gael Bigirimana na Lazarus Kambole hawakuwa sehemu ya mchezo huo

Lomalisa na Bigirimana wanaweza kuwa sehemu ya kikosi leo wakati Kambole akiendelea kuimarika kutoka kwenye majeraha aliyopata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc

Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye alicheza kwa dakika chache Jumamosi huenda nae akarejea kwenye safu ya ulinzi wakati safu ya ushambuliaji Fiston Mayele na Stephane Aziz wao wataendeleza pale walipoishia kwenye mchezo dhidi ya Simba

Mawinga Bernard Morrison na Jesus Moloko ndio walibadilisha mchezo dhidi ya Simba kwenye kipindi cha pili

Leo huenda wakaanza pamoja katika mchezo huo ambao Yanga imedhamiria kushinda ili kuanza vyema msimu wa kusaka ubingwa wa 29

Nabi alitua Arusha jana akiwa na kikosi chake kamili tayari kusaka ushindi muhimu katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’