Shirikisho la Mapira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mwamuzi wa kati ni Elly Sasii kutoka jijini Dar es salaam ambaye atasaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Mohammed Mkono kutoka jijini Dar es salaam, mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Mpanga pia kutoka jijini Dar es salaam
Mwamuzi wa akiba ni Ramadhan Kayoko nae kutoka jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE