Tanzania imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya CHAN inayohusu wachezaji wanaocheza ligi za ndani
Abdul Suleiman Sopu alifunga bao pekee la Stars mwanzoni mwa kipindi cha pili akimalizia krosi ya Kibwana Shomari
Ni matokeo ambayo yanaiweka Tanzania kifua mbele kuelekea mchezo wa marudiano ambao uitapigwa Julai 28 katika uwanja huo huo wa Benjamin Mkapa
Tanzania inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga raundi ya pili ambayo watacheza na majirani zao Uganda




ADVERTISE HERE