Manara ataja sababu ya kumtambulisha Aziz Ki saa tisa usiku

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2022
Manara ataja sababu ya kumtambulisha Aziz Ki saa tisa usiku

Usiku wa kuamkia leo Yanga iliwafanya Wananchi na wadau wa soka nchini na nje ya nchi wakeshe wakisubiri utambulisho wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki

Nyota huyo akatambulishwa saa tisa na dakika kumi usiku na kukata kiu ya Wananchi waliokuwa wakisubiri utambulisho wake kwa hamu

Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema lengo la klabu kufanya utambulisho wa Aziz Ki usiku wa manane ilikuwa kuonyesha ukubwa wao tu

Manara amesema walitaka kuionyesha dunia kuwa Yanga inaweza kuugeuza usiku ukawa kama mchana

Takwimu zimedhihirisha kauli ya Manara kwani baada ya Yanga kumtangaza Aziz Ki, ndani ya nusu saa wafuasi zaidi ya 10,000 walishiriki kutoa maoni katika 'post' hiyo

"Kiukweli hatukuwa na sababu yoyote zaidi ya kuonyesha ukubwa wa Yanga,Tulitaka tuwaambie watu, Yanga inaweza kuufanya Usiku mkubwa uwe na Pilika Pillika kama za Mchana au jioni huku Instagram"

"Labda kuweka Tisa na Dakika kumi ina maana tofauti, kama picha inavyojieleza hapo juu. Ndio, Najua Wapo waliotudhihaki na kusema tunaiua mitandao yetu wenyewe"

"Kwa jana ndio tukaambiwa hatufikiri sawa sawa. Wengine walienda mbali zaidi Kwa kutukejeli kwamba tutapata likes na Comments chache mno. Labda sasa watatupa heshma yetu baada ya hizi takwimu za hapo chini"

"Mabibi na Mabwana, Saa Tisa Usiku ,tena ndani ya nusu saa kupata Comments zaidi ya Elf kumi sio jambo dogo. Hakuna Club yoyote Afrika, inaweza kupata Comments kama hizo ndani ya muda huo kwa Utambulisho wa mchezaji tu, Haipo Club hyo na kama ipo ntajiwe hapa"

"Tisa Usiku upate comments Elfu kumi Kwa nusu saa? Ni Yanga Afrikaaaaaaa. Na Kuna wenzetu toka majuzi wana comments Elfu Sita kwa mchezaji tuliyoambiwa atatingisha Dunia!"

"Aziiz Ki keshakusanya Comments 25 Elfu na Ushee kwa Masaa tu, ndugu zangu wao waliweka Mchana kweupeeee, Wanaume tumekandamiza Tisa Usiku, kisha tushawazidi kwa mbaaali," alitamba Manara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’