Hatimaye leo Wanachama wa Yanga wanakwenda kukidhi matakwa ya kikatiba ya klabu hiyo kwa kufanya Uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya
Leo Yanga inakwenda kuchagua Rais, Makamu wa Rais na Wajumbe watano wa Sekretariati
Ni siku muhimu kwa Wanachama/wawakilishi kufanya maamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi ambao wataipeleka Yanga nchi ya ahadi
Wamewasikia wagombea wote katika siku tano za kampeni, kazi ni kwao kuchagua wale wanaofaa
Muhimu kwa Wanachama mliopata dhamana ya kwenda kupiga kura, mfahamu matumaini ya Mamilioni ya Wananchi yako mikononi mwenu hivyo mhakikishe mnatumia vyema uwakilishi wenu kwa kuchagua viongozi bora
Kila la kheri katika uchaguzi unaofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere
ADVERTISE HERE