Wagombea Yanga wafunga kampeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2022
Wagombea Yanga wafunga kampeni

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Yanga, wamehitimisha kampeni zao leo tayari kwa uchaguzi Mkuu ambao utafanyika kesho Jumamosi ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Mwalimu Julius Nyerere

Mgombea pekee wa nafasi ya Urais Injinia Hersi Said mpaka sasa ana zaidi ya asilimia 90 kuwa Rais wa klabu ya Yanga, Wanachama wa Yanga wanatambua kazi kubwa aliyofanya hata kabla ya kufikiria kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa Yanga

Arafat Haji ndiye anayepigiwa chapuo kuwa Makamu wa Rais kwa kuwa amefanya kazi bega kwa bega na Injinia Hersi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita

Arafat anachuana na Mwanamama Suma Mwaitenda, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayemaliza muda wake

Hata hivyo kitendo cha Mwaitenda kupigiwa kampeni na Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally pamoja na Mchambuzi Jemedari Said ni kama kimewapunguzia imani Wanachama wengi kwake

Kesho Wanachama wa Yanga watakuwa na kazi rahisi tu ya kuwachagua Hersi na Arafat kuwa viongozi wao lakini ushindani mkali unatarajiwa kwenye nafasi tano za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’