Jumamosi, Julai 02 2022 mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union utapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo na watawakabili wapinzani wao Coastal Union kwa tahadharai kubwa
Nabi amesema licha ya kupata ushindi dhidi ya Coastal Union katika mechi zote mbili za ligi, huo ni mchezo mwingine ambao una maandalizi tofauti na mshindi wa mchezo huo ataondoka na taji la FA
"Mechi ya kombe iko tofauti, tunaingia kwenye mechi kwa tahadhari kubwa, tunawaheshimu Coastal Union ni timu nzuri lakini sisi tutaingia na mkakati wetu kupata ushindiΒ na kutwaa ubingwa wa FA," alisema Nabi
Katika hatua nyingine, Nabi amempongeza mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole kwa kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC baada ya kufunga mabao 17
Nabi amesema haikuwa bahati kwa Mayele ambaye kwa kiasi amevunjika moyo baada ya kushindwa kuchukua tuzo hiyo kwa baadhi ya mabao yae kukataliwa lakini pia akiongoza mbio za ufungaji bora kwa muda mrefu