Yanga kuikabili Coastal Union kwa tahadhari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2022
Yanga kuikabili Coastal Union kwa tahadhari

Jumamosi, Julai 02 2022 mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union utapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo na watawakabili wapinzani wao Coastal Union kwa tahadharai kubwa

Nabi amesema licha ya kupata ushindi dhidi ya Coastal Union katika mechi zote mbili za ligi, huo ni mchezo mwingine ambao una maandalizi tofauti na mshindi wa mchezo huo ataondoka na taji la FA

"Mechi ya kombe iko tofauti, tunaingia kwenye mechi kwa tahadhari kubwa, tunawaheshimu Coastal Union ni timu nzuri lakini sisi tutaingia na mkakati wetu kupata ushindiΒ  na kutwaa ubingwa wa FA," alisema Nabi

Katika hatua nyingine, Nabi amempongeza mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole kwa kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC baada ya kufunga mabao 17

Nabi amesema haikuwa bahati kwa Mayele ambaye kwa kiasi amevunjika moyo baada ya kushindwa kuchukua tuzo hiyo kwa baadhi ya mabao yae kukataliwa lakini pia akiongoza mbio za ufungaji bora kwa muda mrefu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
59m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’