Wananchi Yanga wamekabidhiwa taji la ligi kuu walilotwaa msimu huu baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare ya bao 1-1
Wananchi wametwaa ubingwa pasipo kupoteza mchezo wowote katika ligi mpaka sasa
Kwa hakika ni mafanikio ambayo Yanga wamestahili, huu ulikuwa msimu wao
Tangu walipochukua usukani wa ligi kwenye raundi ya tatu, hawakushuka mpaka kutwaa ubingwa
Shamra shamra zinaanzia mkoani Mbeya na zitahitimishwa jijini Dar es salaam kesho Jumapili
Hongera Wananchi kwa kutwaa ubingwa wa 28 ligi kuu ya Tanzania Bara

ADVERTISE HERE