Kesho Jumatano Juni 22 2022 Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza mechi ya mwisho nyumbani wakiikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Yanga imetangaza viingilio vya mchezo huo huku Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao katika mchezo huu wa mwisho nyumbani
VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Muda wa mchezo ni saa 12:30 jioni

ADVERTISE HERE