Wacongomani Yannick Bangala na Djuma Shabani wanatarajia kuongeza mikataba katika klabu ya Yanga
Nyota hao ambao wamebakiza mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja, wamekuwa na wakati mzuri sana kwenye kikosi cha Yanga msimu huu
Ni wazi Yanga imejipanga kuwashikilia wachezaji wake muhimu hasa ikizingatiwa Wananchi wana malengo ya kufanya vizuri katika michuano ya Kimataifa msimu ujao

Hivi karibuni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa aliweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji Fiston Mayele licha ya kupokea ofa kutoka klabu za RS Berkane na Kaizer Chiefs
"Tuna malengo ya kufanya vizuri ligi ya mabingwa msimu ujao hivyo hatuwezi kuwauza wachezaji wetu muhimu. Kupata fedha ni jambo moja lakini kuheshimu mashabiki ni jambo jingine. Kama tukimuuza Mayele tutawaeleza nini mashabiki wa Yanga?," alisema Senzo