Hersi anasubiri kuthibitishwa tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2022
Hersi anasubiri kuthibitishwa tu

Licha ya kuwepo majina makubwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Rais wa klabu ya Yanga, anayezungumzwa zaidi ni mtu mmoja tu, Injinia Hersi Said

Baada ya tetesi kuwa Mjumbe huyo wa Kamati ya Mashindano angejitosa kugombea, jana jioni saa chache kabla ya muda wa kurejesha fomu kutimia, Mzee Mohammed Msumi akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela wakawasilisha fomu ya Injinia Hersi

Lilikuwa tukio lililopokewa kwa shangwe na nderemo na mashabiki wa Yanga

Hersi amejijengea heshima ya kipekee tangu alipoingia katika harakati za kuisaidia Yanga

Alitambulishwa kwa mara ya kwanza na GSM baada ya lile tukio la Kubwa Kuliko, GSM wakichangua Tsh Milioni 300

Baadae GSM wakashinda zabuni ya kutengeneza na kusambaza jezi za Yanga, hapo ndipo Hersi akaanza kufahamika

Hersi akawa msimamizi wa miradi yote iliyokuwa ikifanywa na GSM kwa klabu ya Yanga kwa mujibu wa makubaliano

Jina la Hersi likaanza kuchomoza kwenye michakato ya usajili msimu uliopita akisafiri DR Congo kuwanunua Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda kunako klabu ya AS Vita

Ni katika msimu huo Hersi alisimamia usajili wa wachezaji kama nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Farid Mussa, Yacouba Songne, Haruna Niyonzima na wengineo

Msimu uliopita akafanya mambo makubwa zaidi kwa kumleta Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa akitokea klabu ya Simba pia akiwaleta akina Fiston Mayele, Yannick Bangala, Djigui Diarra, Djuma Shabani, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Heritier Makambo bila ya kumsahau Salum Abubakar 'Sure Boy'aliyetua kwenye usajili wa dirisha dogo

Ni usajili ulioleta mafanikio makubwa msimu huu kwani Wananchi wanakwenda kutwaa ubingwa wa ligi kuu baada ya kuukosa kwa misimu minne

Yanga pia imetinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam wakiwa pia wametwaa Ngao ya Jamii

Lakini kubwa zaidi ni kusimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji sasa Yanga ikianza kunufaika na matunda ya mabadiliko hayo juzi wakitangaza kukusanya Tsh Bilio 1.07 katika kipindi cha miezi sita tu

Hersi ameipambania Yanga, shukrani nyingi zitakwenda kwa GSM ambao ndio waliowezesha yote aliyoyafanya

Haishangazi kuona Mashabiki na Wanachama wamefurahi baada ya Hersi kuchukua fomu na hakuna shaka ATASHINDA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17m ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’