Stars kuikabili Algeria leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jun 2022
Stars kuikabili Algeria leo

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo saa moja usiku itashuka kunako uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Algeria katika mchezo wa kuwania tiketi ya michuano ya Afcon 2023 itakayofanyika nchini Ivory Coast mwakani

Huu ni mchezo muhimu kwa Tanzania kupata ushindi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu Afcon kwa mara ya tatu

Algeria ni moja ya vigogo wa soka barani Afrika, mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2019 wakitwaa taji kule Misri

Leo wanachuana na Tanzania bila ya uwepo wa nyota wao Riyad Mahrez anacheza Manchester City. Mahrez hakujumuishwa kwenye kikosini kwa kuwa ni majeruhi

Algeria wana uzoefu wa michuano mikubwa lakini hilo halipaswi kuwatisha Watanzania kwani wao watakuwa 11 pamoja na mashabiki ambao wameaswa kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa

Mara ya mwisho Algeria kucheza uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Tanzania, mchezo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Ushindi kwa Tanzania leo unaweza kuwapeleka kileleni mwa kundi F kutegemeana na matokeo ya mchezo kati ya Uganda dhidi ya Niger

Kila la Kheri Tanzania, kila la kheri Taifa Stars

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’