FT : Niger 1-1 Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2022
FT : Niger 1-1 Tanzania

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuondoka na alama moja muhimu huko Benin baada ya kulazimisha matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Niger katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2023

Tanzania ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya kwanza kupitia kwa George Mpole ambaye alimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Niger baada ya shuti la Saimon Msuva

Niger walirejea mchezoni kwenye dakika ya 26 wakisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Sosah

Pamoja na Niger kumiliki mchezo kwa muda mwingi, Stars walikuwa hatari zaidi kwenye mashambulizi ya kushitukiza Kibu Denis akikaribia kufunga bao la ushindi kama shuti lake kugonga mwamba baada ya mlinzi wa Niger kufanya makosa kwa kumrudishia mlinda lango wake pasi fupi

Ni alama moja muhimu kwa Tanzania kuelekea mchezo wa pili dhidi ya Algeria ambao utapigwa Juni 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’