Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinaondoka nchini leo kuelekea Benin wanakokabiliwa na mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Niger
Niger itacheza mechi zake za nyumbani huko Benin baada ya uwanja wao wa nyumbani kutokidhi vigezo wakianza na mchezo dhidi ya Stars ambao utapigwa Jumamosi, Juni 04
Stars itaondoka nchini kwa usafiri wa ndege maalum ambayo itawarejesha Tanzania baada ya mchezo
Tanzania inakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya Algeria ambao utapigwa Juni 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE