Rais Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwekeza katika mpira ili timu za Tanzania ziweze kufanya vizuri kimataifa.
Rais Samia ameyasema hayo jana Mei 31, 2022 akipokea Kombe la Dunia litakalowaniwa Qatar baadae mwaka huu.
"Timu ya wanawake na wadogo inafanya vizuri, huku kwingine mnaanza vizuri lakini hammalizii viuzri, Wizara naomba muwekeze," amesema na kuongeza
"Kombe hili liwe chachu ya kufanya vizuri sio kwa kutetema na kunyunyiza ni ufundi mguuni, kama kutetea na kunyunyiza inasaidia fanyeni lakini ufundi zaidi"
Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Wizara kuwekeza zaidi na kwamba upande wa serikali wameanzisha mfuko wa michezo ambao tayari wameanza kuwekeza fedha na kwamba mwaka huu serikali itajitaidia kuutafutia fedha ili ziweze kusaidia katika uwekezaji wa kutayarisha timu za vijana.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopata nafasi kupitiwa na ziara za kombe la Dunia
