Ushindi dhidi ya Simba 'utanogesha' ubingwa - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2022
Ushindi dhidi ya Simba 'utanogesha' ubingwa - Senzo

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa amesema umekuwa msimu mzuri baada ya kufanikiwa kuwavua taji, Simba huku wakiwafunga mara mbili msimu huu.

Jumamosi iliyopita, Yanga iliichapa Simba bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Senzo ambaye pia amewahi kuwa Mtendaji Mkuu Simba amesema baada ya kuwakosa mara mbili katika Ligi Kuu Bara mechi zote zikiisha kwa suluhu sasa wanaenda kulisaka taji la pili la ASFC kupitia mgongo wa Simba.

"Soka la Tanzania unataka vitu vya namna hii mashabiki wetu walikuwa kila wakati wanaumia wakituambia wanatamani kuona tunawafunga Simba, angalau mechi moja kisha tuchukue ubingwa"

"Hapa nadhani sasa watafurahia kama ambavyo uongozi tunafurahia na wadhamini wetu wote,huu ushindi unaleta nguvu kwetu tukichukua mataji mbele ya ushindi kwao,hapa sasa ubingwa unakuwa mtamu," alisema Senzo

Senzo amesema Yanga haijamaliza kazi watashuka na nguvu kubwa kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Coastal Union ili kuhakikisha wanashinda taji hilo.

"Tunaishi katika malengo yetu,tulijipanga kuhakikisha tunashinda hii mechi dhidi ya Simba lakini sasa tumetinga fainali huko sasa tutaingia kwa nguvu zaidi bila kuangalia tunakutana na nani,hii ni fainali lazima iwe na ugumu wake na sio kudharau"

"Tuna wachezaji bora na benchi bora la ufundi chini ya Kocha Nabi (Nasreddine) tutawasikiliza wanachotaka na uongozi tutayafanyia kazi tunalitaka hili komb la pili pia"

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’