Winga wa Yanga Dickson Ambundo anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kuomba radhi kufuatia makosa aliyofanya ambayo yalipelekea aondoshwe kambini kuelekea mchezo dhidi ya Simba uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita
Ambundo amesamehewa baada ya kukiri na kuomba msamaha katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga jana
Ambundo anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake siku ya Alhamisi kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Jana Yanga ilitangaza kuachana na kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye alisimamishwa pamoja na Ambundo
Saido alipaswa kushiriki kikao hicho lakini yeye aliondoka kuelekea kwao Burundi baada ya uongozi kumuondoa kambini mkoani Shinyanga
Mkataba wake ulifika tamati jana lakini Yanga imesitisha mpango wa kumuongezea mkataba mwingine