Rostand awatuliza mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2018
Rostand awatuliza mashabiki Yanga
kipa wa Yanga, Youthe Rostand, amesema mashabiki waliokuwa wakibeza uwezo wake watulize mzuka kwani amepanga kufanya makubwa hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Rostand amesema anatambua kwamba mashabiki walikuwa wameanza kukosa imani naye hasa katika upande wa penalti, hivyo alikuwa akijifua ili kuwa fiti na kumaliza tatizo hilo.

Kipa huyo aliibeba Yanga kwenye mikwaju ya penalti dhidi ya Ihefu FC katika Kombe la FA ambapo sasa wametinga hatua ya 16 Bora.

"Siku zote likitokea jambo baya huwezi kulijibu kwa maneno, inabidi uwajibu kwa kusahihisha lile tatizo ambalo lilizua maneno. Nashukuru Mungu zoezi langu limeanza kukamilika kidogo kidogo, nitakuwa nafanyia kazi zaidi,"alisema.

"Tunajua kwamba mashabiki wanataka matokeo mazuri muda wote, tutahakikisha tunapambana ili tuweze kusonga mbele katika mashindano ya kimataifa. Mimi, Kabwili (Ramadhani) na Kakolanya (Beno) wote tupo vizuri katika kulinda lango, hivyo hatutowaangusha, hata wachezaji wengine nao wanafanya vizuri kwenye nafasi zao, tutatumia mashindano haya kujitangaza," aliongeza Rostand katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’