Msemaji wa Yanga Haji Manara amevunja ukimya kuhusu tetesi zinazoendelea kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mchezaji Bernard Morisson anayehusishwa na mabingwa hao watarajiwa wa ligi kuu ya NBC
Manara amekanusha taarifa iliyoripotiwa na Mwanahabari Jemedari Said kupitia ukurasa wake wa Instagram akidai Yanga imeshamalizana na Morrison
Manara amesema Yanga haikuwahi kuzungumza na Morrison, huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo wajikite zaidi kwenye harakati zao za ubingwa wa 28 na mchezo unaofuata wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, May 28
"Huyo Morrison ni mchezaji wa Simba, sisi hatujazungumza nae mahali popote. Hizi ni propaganda zinazofanywa na wenzetu tu, mashabiki wetu wasiingie katika mtego huu. Tujikite zaidi kwenye kushinda ubingwa wa ligi kuu na kombe la FA"
"Masuala ya usajili tutayazungumza baada ya msimu kumalizika. Kwa sasa itoshe kusema hatujazungumza na Morrison," alisema Manara