Wananchi wametakata uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma jioni ya leo wakiichapa Dodoma Jiji mabao 2-0 katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali
Mabao ya mashuti ya nje ya 18 yaliyopigwa na Dickson Ambundo na Zawadi Mauya yaliihakikishia Yanga kupata alama hizo tatu muhimu
Licha ya changamoto ya uwanja wa Jamhuri, Yanga ilitawala mchezo kiungo Abubakar Salum 'Sure Boy' akiihakikishia Yanga umiliki mkubwa wa mpira kwenye eneo la kiungo
Pengine Yanga ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kama Dickson Ambundo na Denis Nkane wangetumia nafasi adimu walizopata kwenye kipindi cha pili
Ushindi huu unaifanya Yanga iendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi wakifikisha alama 60, Wananchi wanahitaji alama 11 tu kutoka kwenye mechi sita zilizobaki kujihakikishia ubingwa
Matokeo haya ni zawadi na pole kwa Yannick Bangala ambaye licha ya kufikwa na kaka yake aliweza kuingia katika kipindi cha pili na kuisaidia Yanga kupata matokeo haya





