Michezo ya Kimataifa kuvuruga ratiba za Yanga, Simba VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jan 2018
Michezo ya Kimataifa kuvuruga ratiba za Yanga, Simba VPL
Ligi Kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii ambapo vilabu vya Yanga na Simba vinavyoshiriki michuano ya Kimataifa vitashuka dimbani.

Yanga itacheza Jumamosi, February 03 ikiwa ugenini mkoani Iringa dhidi ya Lipuli FC wakati Simba itakuwa uwanja wa Taifa kumenyana na Ruvu Shooting.

Baada ya mchezo huo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani Februari 06 kuivaa Njombe Mji kwenye uwanja wa Taifa huku Simba ikitarajiwa kupepetana na Azam FC Februari 07.

Ikumbukwe Yanga itakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis Februari 10 huku Simba ikichuana na Gendermerie mchezo wa kombe la shirikisho Februari 11.

Kuna taarifa kuwa uongozi wa Simba umeiandikia barua TFF kuiomba iahirishe mchezo wake dhidi ya Azam FC ili iweze kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho.

Kama TFF itakubali maombi hayo ya Simba basi italazimika kuahirisha na mchezo wa Yanga dhidi ya Njombe Mji pia ili nayo ijiandae ipasavyo kuikabili St Louis.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
2h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
14h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
23h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’