Jana TP Mazembe ilicheza na RS Berkane mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali kombe la Shirikisho barani Afrika, mchezo ambao uliwakutanisha wachezaji wa zamani wa Yanga, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na Fiston Abdulrazak
Ilikuwa furaha kwa Mukoko kukutana na Tuisila na Fiston ambao wote waliitumikia Yanga msimu uliopita
Licha ya kuondoka Tanzania, nyota hao bado wana mapenzi makubwa kwa Yanga
Kisinda aliwahi kuweka bayana kuwa anatamani kurejea tena Yanga kwani kazi iliyokuwa imemleta Tanzania hakuikamilisha!



ADVERTISE HERE