Baadae leo, majira ya saa moja usiku Yanga itakuwa dimba la Benjamin Mkapa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC raundi ya 23
Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kupata alama zote tatu ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushangilia timu yao
Bumbuli amesema Yanga inaendelea na mkakati wake wa ubingwa ambao ni kushinda michezo yote mitano inayofuata, mechi ya Prisons ni moja wapo


ADVERTISE HERE