Ni wazi mshambuliaji wa Yanga Chico Ushindi anaweza kuwa kwenye wakati mgumu pale msimu utakapofika tamati kutokana na mfululizo wa majeraha yanayomsumbua
Tangu aliposajili dirisha dogo akitokea klabu ya TP Mazembe, Ushindi hajaonekana kwa muda wa kutosha uwanjani kutokana na changamoto ya majeraha ya kila mara
Imeelezwa moja ya kigezo ambacho Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameweka kwa wachezaji anaowahitaji katika kikosi chake msimu ujao, ni wale ambao watampa uhakika wa kutumika mara nyingi pale wanapohitajika
Wakati Yanga inamsajili Ushindi kutoka TP Mazembe ilikuwa na matumaini kuwa nyota huyo atapona majeraha yake na kuisaidia timu katika vita ya ubingwa msimu huu
Hata hivyo imekuwa tofauti, Ushindi amekuwa nje akitibiwa zaidi kuliko muda aliotumika uwanjani