Tumejipanga kuikabili Ruvu Shooting - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 May 2022
Tumejipanga kuikabili Ruvu Shooting - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wamejiandaa kukabiliana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma

Kaze amesema wanafahamu mchezo hautakuwa mwepesi kwa kuwa mechi zote wanazokutana na Ruvu Shooting zinakuwa na upinzani mkali

Hata hivyo amesema wamewaandaa wachezaji kimwili na kiakili kuweza kupata matokeo dhidi ya Ruvu Shooting hasa wakizingatia wanatoka kwenye mchezo mgumu dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi iliyopita na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Kaze amesema watatumia wachezaji bora zaidi kwenye kila nafasi ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri

"Tumekuwa tukifanya mazoezi ya kupoza miili baada ya kutoka kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao nguvu nyingi ilitumika. Tumewaandaa wachezaji kuwakabili Ruvu Shooting katika mchezo ambao utakuwa mgumu"

"Ruvu Shooting wana timu nzuri na mara nyingi wametupa upinzani katika michezo tuliyokutana nao. Ni mchezo ambao tutahitaji kutumia wachezaji wetu bora katika kila nafasi ili tuweze kupata matokeo mazuri," alisema Kaze

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’