Daktari wa Yanga Dk Shecky Mngazija amethibitisha kuwa wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kulikuwa na hofu kwa Wananchi kuhusu hali ya mlinzi wa kulia Djuma Shabani ambaye alishindwa kumaliza mchezo uliopita dhidi ya Namungo Fc na akakosa siku kadhaa za mazoezi
Mngazija amesema wachezaji wote wako tayari, kazi imebaki kwa Kocha Nasreddine Nabi kuamua awatumie wachezaji gani katika mchezo huo
"Hatuna majeruhi, wachezaji wote wanafanya mazoezi kuelekea mchezo wa Jumamosi wakiwa na ari kubwa. Limebaki jukumu la Mwalimu kuamua nani aanze katika mchezo dhidi ya Simba," alisema Mngazija
Yanga ndio wenyeji wa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini
Wananchi wanahitaji ushindi ili kuzidi kuukaribia ubingwa wa ligi kuu msimu huu