Twendeni tukaujaze uwanja wa Mkapa - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Apr 2022
Twendeni tukaujaze uwanja wa Mkapa - Manara

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wananua tiketi siku ya leo na kesho kuepuka usumbufu siku ya mchezo

Manara amesema wamekusudia kufunga zoezi la mauzo ya tiketi siku ya Ijumaa, Jumamosi ni siku ya kwenda uwanjani kuishangilia timu yao katika mchezo dhidi ya Simba kuhakikisha wanashinda mchezo huo

"Napenda niwakumbushe mashabiki wetu, tuna siku mbili tu zimebaki, hakikisheni mnanua tiketi zenu mapema. Nimepewa taarifa na Mkurugenzi wa fedha kuhusu mwenendo wa mauzo ya tiketi, 'kumechafuka' hakikisha unanunua tiketi yako mapema"

"Tungependa kuona sisi Yanga tukiwa wenyeji wa mchezo huo, tunakuwa na mashabiki wengi uwanjani, angalau katika mashabiki watatu wanaokwenda uwanjani, wawili wawe ni Yanga tena wakiwa wamevalia jezi zao"

"Tunayo ofa kwa Tsh 25,000/- utajipatia jezi ya msimu huu 2021/22 pamoja na tiketi ya mzunguuko na Tsh 15,000/- utajipatia jezi ya msimu uliopita pamoja na tiketi ya mzunguuko"

"Twendeni uwanjani kwa wingi ili tukawaunge mkono wachezaji wetu ambao wametupa jeuri ya kutamba msimu huu," alisema Manara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’