Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la vijana klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amerudishwa tena kuwa kocha msaidizo wa timu ya Taifa ya DR Congo.
Taarifa iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Congo ni imesema Zahera anarudi katika kikosi hicho akimsaidia Muargentina Hector Cuper.
Zahera anachukua nafasi ya kocha Daouda Lupembe ambaye ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata kazi katika timu ya Sanga Balende inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
"Nimepata hizo taarifa ni furaha kubwa kwangu kurudi katika majukumu ya kumsaidia kocha mkuu (Cuper) lakini kikubwa ni kurudisha nguvu ya taifa letu baadea ya kukosa Fainali za Kombe la Dunia,"alisema Zahera
ADVERTISE HERE