Yanga yatahadharishwa mchezo dhidi ya Ihefu FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jan 2018
Yanga yatahadharishwa mchezo dhidi ya Ihefu FC
Tofauti na misimu iliyopita, msimu huu michuano ya kombe la FA imekuwa na ushindani mkali kutokana na kila timu kujiandaa kikamilifu.

Mwezi uliopita tumeshuhudia mabingwa watetezi wa michuano hiyo Simba wakitolewa na timu ya daraja la pili Green Worriors.

Aidha Yanga ilifanikiwa kupenya dhidi ya Reha FC kwenye mchezo wake wa kwanza. Hata hivyo ililazimika kusubiri dakika 10 za mwisho kupata ushindi wa mabao 2-0.

Leo itaivaa Ihefu FC, timu kutoka Mbalali mkoani Mbeya ambayo inashiriki ligi daraja la pili Taifa.

Ihefu ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha timu inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom, ndugu zao Mbeya City.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Sokoine kuanzia saa kumi kamili jioni leo Jumanne Januari 30, unatarajiwa kuwa mgumu na Yanga itahitaji kuingia kwa tahadhari kubwa.

Ihefu FC imekamia mchezo huo, njia pekee ya Yanga kuibuka na ushindi ni kuhakikisha inashusha silaha zake za maangamizi kwani michuano ya msimu huu jambo lolote linaweza kutokea.

Yanga tayari iko jijini Mbeya ambapo baadhi ya viongozi na wachezaji wachache waliondoka na basi jana huku kikosini kamili kikikwea pipa Alfajiri ya leo.

Ikumbukwe baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16 dhidi ya Lipuli FC.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’