Yanga ya Kimataifa yaanza kusukwa mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2022
Yanga ya Kimataifa yaanza kusukwa mapema

Mpaka sasa Yanga ina uhakika wa zaidi ya asilimia 80 kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao

Wananchi wanahitaji kushinda michezo angalau mitatu ili kujihakikisha kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi

Azam Fc ambao wako nafasi ya tatu, wameachwa alama 23 na Yanga wakati Namungo Fc waliko katika nafasi ya nne wameachwa alama 25!

Lakini lengo la Yanga ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi kuu wakiwa juu ya msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10

Mabosi wa Yanga tayari wameanza michakato ya kubaini wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa ili kuongeza nguvu kwenye michuano ya Kimataifa msimu ujao

Moja ya maeneo ambayo yanatarajiwa kuongezewa nguvu ni kwenye safu ya ulinzi, Yanga ikitajwa kumuwania mlinzi wa kati wa Ghana anayecheza klabu ya Asante Kotoko, Yussif Mubarik

Yussif amekuwa na kiwango bora akiwa katika msimu wa pili akiitumikia Kotoko

Habari za ndani zimedokeza kuwa mchezaji huyo ni pendekezo la kocha Nasreddine Nabi

Lakini kama haitakuwa rahisi kumpata, Wananchi wanaweza kuhamia kwa Mkenya Joash Onyango ambaye anamaliza mkataba na Simba

Hivi karibuni Msemaji wa Yanga Haji Manara alidokeza wachezaji 11 wa Simba wanamaliza mikataba mwishoni mwa msimu na wapo baadhi yao wamepiga hodi GSM wakiomba wapewe mikataba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
33m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’