Ubingwa wa ligi kuu ni suala la muda tu - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2022
Ubingwa wa ligi kuu ni suala la muda tu - Manara

Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema anaamini ni suala la muda tu Yanga itatangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya NBC msimu wa 2021/22

Akizungumza katika tukio la futari lililoandaliwa na GSM jana, Manara alisema ubora wa kikosi cha Yanga unawapa kila sababu ya kuamini watatwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

"Kuna mwandishi mmoja kaandika makala ndefu akidai kuwa GSM na Yanga wanafanya matukio mengi ya charity kwa sababu wanautaka ubingwa. Ukweli ni kuwa ubingwa tunao tu, matukio haya tunayafanya kwa sababu tumeona kuna wenzetu wanahitaji kusaidiwa na pia ni jambo jema kwani tunafahamu yana malipo kutoka kwa Mwenye ez Mungu"

"Kuhusu ubingwa ni suala la muda tu, pengine tunasubiri mwezi mmoja na wiki moja au mbili, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mzee Mnguto atatuandikia barua kutuuliza ni wapi angependa tukakabidhiwe kombe letu. Jamani kwa Yanga hii yenye kina Aucho na Bangala tunawezaje kukosa ubingwa?," alitamba Manara

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC ikiwa na alama 51 baada ya kushuka dimbani mara 19 ikifuatiwa na Simba yenye alama 41 pia ikicheza michezo 19

Kimahesabu Wananchi wana nafasi kubwa ya kuwa mabingwa, katika michezo 11 iliyobaki, wanahitaji kushinda michezo nane tu 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’