Juzi katika mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold, mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra alidhihirisha thamani yake baada ya kuisaidia Yanga kutinga nusu fainali ya michuano hiyo
Ni moja ya mechi ngumu ambazo Yanga wamecheza msimu huu, ushindi ulichangiwa na uhodari wa mlinda lango huyo
Baada ya kukosa mkwaju wa penati, ilionekana kama safari ya Yanga kwenye michuano hiyo ingeishia hatua ya robo fainali
Lakini Diarra akasahihisha makosa yake kwa kuokoa mkwaju wa Juma Mahadhi huku akiusindikiza nje ya lango mkwaju wa Maka Edward
Injinia Hersi Said hakubahatisha kwenda Mali kuifuata saini yake
Mpaka sasa Diarra ndiye kinara wa cleansheet kwenye ligi (10) licha ya kukosa mechi kadhaa alipokwenda kushiriki michuano ya Afcon mwezi Februari 2022 akiwa na Mali



