Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ameeleza kushangazwa na kauli zilizotolewa na Afisa Habari mwenzake wa Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' kuhusu mshambuliaji Fiston Mayele
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Zakazakazi aliandika Makala akieleza kuwa Mayele sio mshambuliaji tishio (ni wa kawaida) akitoa mifano ya washambuliaji waliocheza ligi kuu miaka ya nyuma
Ikumbukwe Mayele ameifunga Azam Fc katika michezo yote miwili ya ligi kuu ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex hivi karibuni
Bumbuli amehoji Mayele amemkosea nini Zakazakazi hadi kufikia kuandika makala ndefu kuelezea jinsi alivyo mchezaji wa kawaida
ADVERTISE HERE