Unamkumbuka yule mlinzi wa Simba Hennock Inonga alichofanya kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana?
Wakati Mayele akitoka nje kumpisha Heritier Makambo, Inonga alimsindikiza huku akijinasibu kuwa amemzuia asiteteme katika mchezo huo
Mayele amelizungumzia tukio lile lakini amesema kwake ni deni kubwa ambalo anapaswa kulilipa
"Yule ni rafiki yangu, sijui kichwani mwake alikuwa akifikiria nini lakini nikwambie lile ni deni kwangu lazima nilipe, Nina deni na watu wawili (timu), Namungo Fc na Simba," alisema Mayele
Simba na Namungo Fc ni miongoni mwa timu sita ambazo Mayele hajazifunga kwenye ligi ingawa Simba aliifunga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii
Timu nyingine ambazo Mayele hakufunga ni dhidi ya Tanzania Prisons, Polisi Tanzania, Mbeya City na Ruvu Shooting
Mchezo unaofuata kwenye ligi ni dhidi ya Simba ukipigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kwa Mayele hiyo itakuwa siku ya kulipa deni!