Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wachezaji viraka Yannick Bangala na Farid Mussa wanaweza kuukosa mchezo dhidi ya Azam Fc hapo kesho kutokana na changamoto zinazowakabili
Akizungumza utayari wa kikosi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc hapo kesho, Kaze amesema Bangala alipata majeraha mazoezini juzi ambapo jana alishindwa kufanya mazoezi

Aidha Farid ameugua ghafla ambapo wanaendelea kuangalia hali yake kuelekea mchezo huo
Kaze pia amewataja viungo Khalid Aucho na Feisal Salum 'Fei Toto' kuwa wataukosa mchezo huo kutokana na majeraha yanayowakabili
Yanga imeendelea kukumbwa na changamoto ya majeruhi ambayo si jambo jema sana katika kipindi hiki ambacho Wananchi wako katika mapambano makali ya kuwania ubingwa wa ligi kuu
ADVERTISE HERE